28 Jan 2020 / 364 views
Thomas Ulimwengu arudi TP Mazembe

Klabu ya soka ya TP Mazembe imetangaza kumrejesha mshambuliaji Thomas Ulimwengu kwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Ulimwengu amerejea Mazembe ambako aliondoka mwaka 2016 kwenda kutafuta mafanikio mengine ya soka barani Ulaya, ambapo alijiunga na klabu ya FC Athletic Eskilstuna kisha FK Sloboda Tuzla kati ya mwaka 2017-18.

Mwaka 2018 alirejea barani Afrika ambapo alijiunga na klabu ya Al Hilal Omdurman ya nchini Sudan ambayo inashiriki michuano ya Afrika.

Baadaye mwaka 2019 Ulimwengu alijiunga na klabu ya JS Saoura ya Algeria ambapo alicheza katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na kikosi hicho.

Ulimwengu anarejea kuimarisha safu ya ushambuliaji ya TP Mazembe, ambapo anatarajia kutua mjini Lubumbashi Jumatano kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.