12 Dec 2019 / 245 views
Bayern yashinda mechi zote sita Uefa

Klabu ya Bayern Munich imekuwa klabu ya kwanza ya Ujerumani kushinda mechi zote sita za hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda 3-1 dhidi ya Tottenham.

Bayern Munich na Tottenham wote wawili walikuwa tayari wameshafuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo lakini walikuwa wanakamilisha hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Kingsley Coman alikuwa wa kwanza kuwapatia Bayern Munich goli la kwanza dakika 27 kwenye mechi hiyo ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Ingawa kijana Ryan Sessegnon alisawazisha na bao lake la kwanza kwa Spurs, Bayern akashinda goli la pili kupitia Thomas Mueller na mpaka kipindi cha kwanza Bayern Munich alikuwa anaongoza mechi hiyo.

Goli la tatu la Bayern Municch lilifungwa na Philippe Coutinho na kufanya matokeo kuwa 3-1 kwenye mechi hiyo ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Bayern iliifunga Tottenham 7-2  kwenye mechi ya kwanza na matokeo ya mechi mbili kuwa 10-3 kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo ya klabu bingwa Ulaya msimu huu.

Kwenye mechi hiyo, Mourinho alipumzika nyota kadhaa na Lucas Moura akichukua nafasi ya mshambuliaji wa Uingereza, Harry Kane.