05 Nov 2019 / 397 views
Ratiba ya UEFA leo

Michuano ya klabu bingwa Ulaya (UEFA Champions League) inaendelea tena leo kwa michezo saba itakayopigwa katika viwanja tofauti barani humo.

Chelsea watakuwa nyumbani katika dimba la Stamford Bridge wakawaribisha mabingwa wa Uholanzi Ajax ambapo kwenye mechi ya kwanza kati ya timu hizo iliyofanyika wiki mbili zilizopita Chelsea waliibuka na ushindi wa goli 1-0.

Baada ya kupoteza mechi ya ligi dhidi ya Levante, Barcelona leo watakuwa nyumbani wakicheza dhidi ya Slavia Prague kutoka Jamhuri ya Cech ambapo kwenye mechi ya kwanza Barcelona walishinda 2-1.

Genk ya Mbwana Samatta leo itashuka dimba la Anfield kumenyana na bingwa mtetezi wa Ulaya Liverpool ambapo kwenye mechi ya kwanza Liverpool walishinda 4-1.

Ratiba kamili leo ipo kama ifuatavyo

Chelsea vs Ajax

Barcelona vs Slavia Prague

Liverpool vs Genk

Napoli vs RB Salzburg

Borussia Dortmund vs Inter Milan

Lyon vs Benfica

Zenit vs RB Leipzig

Valencia vs Lille