1. Vigezo na Masharti:
 1. Huduma hii ni kwa ajili ya wateja wa Tigo wa malipo ya awali.
 2. Kampeni hii kufanyika kuanzia tarehe 4 septemba 2019 hadi 5 Decemba 2019
 3. Tarehe ya kumalizika kwa kampeni inaweza kubadilika kwa kutegemea muenendo wa utoaji wa Zawadi.
 4. Kila mteja anayeshiriki kampeni hii, anaweza kushinda endapo tu atakusanya point nyingi Zaidi ya wengine kwa kujibu maswali ya mpira. Kila swali mteja atakalopokea atagharamia Tsh 99.

 

 1. Jinsi ya kuchagua WASHINDI;
 1. Zawadi za kila siku, Kila wiki na kila mwezi zitatolewa kwa washindi baada ya kushiriki kwenye kampeni kwa kupitia namba husika ya SMS (15670) na kukusanya point Zaidi.

 

Muwakilishi wa Idara ya Bahati Nasibu (Gaming Board) lazima awepo pindi Mshindi anapotafutwa/kutajwa au kupigiwa simu.

 

Kila unavyozidi kujibu maswali ndio unayojiongezea point na nafasi ya kushinda kwa kuwa na point nyingi INAONGEZEKA. Ukijibu Zaidi ndio nafasi ya KUSHINDA inaongezeka.

 

Washindi wote wa SIKU, WIKI na MWEZI watachaguliwa kulingana na point walizokusanya. Mteja atakayekuwa amekusanya point Zaidi ya wengine ndani ya muda Fulani ndiye atakayechaguliwa kuwa Mshindi.

 

 1. ZAWADI;
 1. ZAWADI YA MWISHO WA MSIMU: Kutakuwa na Mshindi mmoja (1) wa zawadi                                                                 ya mwisho wa msimu . Mwisho wa msimu mshindi aliekusanya pointi nyingi katika msimu wote wa miezi mitatu atashinda jumla ya milioni kumi na mbili ( 12,000,000)

Mshindi atatangazwa kwa umma ndani ya siku tatu (3) za kazi. Mshindi atachaguliwa tarehe  05/12/2019.

  1. ZAWADI ZA MWEZI: Kutakuwa na Mshindi mmoja (1) wa mwezi kila mwezi kwa jumla ya miezi mitatu (3). Kila mwezi Mshindi kuchaguliwa mwenye point nyingi. Kila mwezi Mshindi atashinda jumla ya Tsh 1,000,000 (Milioni Moja) Kutakuwa na washindi watatu (3) wa mwezi.

Washindi watatangazwa kwa umma ndani ya siku tatu (3) za kazi. Washindi watachaguliwa tarehe zifuatazo;

Mshindi wa mwezi wa Kwanza:               05/10/2019

Mshindi wa mwezi wa Pili:                       05/11/2019.

Mshindi wa mwezi wa tatu:                        05/12/2019

 

  1. ZAWADI ZA WIKI:
   1. Cash Prizes:

 Mshindi mmoja (1) wa Zawadi ya wiki kupatikana ambaye atakuwa na point nyingi Zaidi ya wengine ndani ya wiki hiyo ambaye atashinda Tsh 500,000 (Laki Tano). Kutakuwa na washindi KUMI NA MBILI (12) wa zawadi ya kila wiki na watatangazwa ndani ya tarehe zifuatazo;

 

12/9/2019, 19/9/2019, 26/9/2019, 3/10/2019, 10/10/2019, 17/10/2019, 24/10/2019, 26/6/2019, 31/10/2019, 7/10/2019, 14/10/2019, 21/10/2019, 28/10/2019.

 

  1. ZAWADI ZA SIKU:  Kila siku kutakuwa na Washindi sita (6) wa fedha taslim shilingi elfu Hamsini (Tsh 50,000) kwa mtu mmoja na elfu kumi (10,000) kwa watu watano. Baada ya kukusanya point nyingi zaidi ndani ya siku hiyo. Kutakuwa na jumla ya washindi 540 wa Zawadi ya siku.

 

 1. Washiriki wote wa kampeni hii ni lazima wawe na miaka 18 na Zaidi.
 2. Mteja anaweza kujiunga kwenye huduma kwa kutuma neno SOKA kwenda 15670. Kujiunga ni bure na baada ya hapo mteja atapokea maswali yanayouhusu mpira. Kila swali atakalopokea litamgharimu Tsh 99.
 3. Neno lolote ( isipokuwa A au B) litakalotumwa kwenye namba 15670 litajumuishwa kama jibu lisilo sahihi kwa swali lililopita. Mfumo utatuma SMS ya swali linalofuata kama mteja ana salio la kutosha.
 4. Kila jibu sahihi mteja atapokea point MIA MOJA (100) na lisilo sahihi mteja atapokea point Ishirini na tano (25)
 5. Ili kupata nafasi ya kushinda, mteja anapaswa kujibu maswali ya mpira kuongeza nafasi yake ya ushindi.
 6. Mteja anapojibu maswali mengi zaidi ndio anajiongezea pointi na anapata nafasi ya kujiongezea USHINDI
 7. Washiriki wote wa kampeni wana nafasi sawa ya KUSHINDA, Ukijibu Zaidi ndio unajiongezea nafasi ya KUSHINDA kwenye kila droo.
 8. Kujitoa katika huduma mteja anatakiwa kutuma neno ONDOA SOKA kwenda 15670.
 9. HAKUNA gharama za kujitoa katika huduma.
 10. Mshindi yeyote ambaye hatopokea simu/ Simu yake Haitopatikana kipindi cha kujulishwa Mshindi mara 3 basi nafasi hiyo ITAONDOLEWA kwake na kupewa Mshindi anayefuata mwenye point nyingi kupigiwa na akipatikana basi huyo ndio MSHINDI!
 11. Mshindi yeyote ambaye alipigiwa simu na hakupatikana/ hakujibu simu mara 3 hatokuwa na ruhusa ya kudai Zawadi hiyo.
 12. Zawadi zote za kampeni ya “ SOKA SMS TRIVIA PROMOTION” zitakabidhiwa katika office za Tigo.
 13.  Kila mteja ananafasi ya kushinda Zawadi ya KIPENGELE FULANI MARA MOJA (1) tu na hairuhusiwi kushinda kipengele hicho tena. Mfano. Mteja akishinda Zawadi ya WIKI ya kwanza, hafai kushinda Zawadi ya wiki kwa wiki inyofuata.
 14.  Tigo itabakia na Zawadi ya Mshindi kwa muda wa miezi mitatu (3) endapo Mshindi huyo hajajitokeza kuichukua Zawadi yako. Baada ya muda huo Mshindi hatokuwa na haki ya kuichukua Zawadi.
 15.  Tigo inaweza kutumia baadhi ya taarifa kama picha, sauti au video za MSHINDI aliyeshinda Zawadi ya kampeni hii kwa kipindi chote cha kampeni kwa ajili ya uhamasishaji wa kampeni.
 16. Jina la Mshindi linaweza kuchapishwa kwenye magazeti au vyombo vingine vya habari.
 17. Waajiriwa wa Green Telecom na Tigo pamoja na familia zao hawaruhusiwi ya kushiriki kwenye kampeni hii.
 18. Kampeni hii ni kwa ajili ya wateja wote wa Tigo ambao ni raia wa Tanzania.
 19. Majina ya washindi yanaweza kutangazwa au kuchapishwa katika vyombo vya habari vilivyochaguliwa na waendesha kampeni.
 20. Kuanzia tarehe 1 Julai 2019 na kuendelea Makato ya ushuru kwa michezo ya Bahati Nasibu kwenye Zawadi zote ni 20%
 21.  Zawadi katika kampeni hii hairuhusiwi kubadilishana, kubadilishwa kwa kupewa mtu mwingine.
 22. Washindi wote wanapaswa kutoa vitambulisho halali. Vitambulisho vifuatavyo kujumuishwa ( Kitambulisho cha NIDA, Kitambulisho cha mpiga Kura au Leseni ya Udereva)
 23. Tigo inauwezo wa kubadilisha vigezo na masharti muda wowote kwa kupeleka mapendekezo yao katika Taasisi ya Kuratibu Mashindano ya Bahati Nasibu (Gaming Board of Tanzania)