24 Jun 2022 / 95 views
Tetesi za usajili Ulaya

Mshambuliaji wa Ajax wa Brazil Antony, 22, 'amedhamiria' kujiunga na Manchester United msimu huu wa joto. Beki wa pembeni wa Manchester United Muingereza Brandon Williams, 21, anaweza kuuzwa kwa £10m.

Ajax wanatazamiwa kuwasilisha ofa nyingine kwa winga wa Tottenham Hotspur na Uholanzi Steven Bergwijn, 24, lakini klabu hiyo ya Premier League haitakubali chochote chini ya pauni milioni 25.

Southampton wamejaribu kuzuia nia ya Manchester City, Manchester United, Tottenham na West Ham kumnunua kiungo wa kati wa England James Ward-Prowse, 27, kwa dau la pauni milioni 75.

Afisa mkuu mtendaji  wa Bayern Munich Oliver Kahn anasema anatarajia fowadi wa Poland Robert Lewandowski, 33, kusalia na mabingwa hao wa Ujerumani msimu huu wa joto.

Manchester City wapo kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kutaka kumsajili beki wa Brighton na Uhispania Marc Cucurella, 23.

Meneja wa Barcelona Xavi anamsihi winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 25, kusaini kandarasi mpya huku Chelsea ikiwindwa na klabu hiyo.

Leeds United wanatazamia kumsajili winga wa PSV Eindhoven wa Uholanzi Cody Gakpo, 23, msimu huu wa joto kama mbadala wa fowadi wa Brazil Raphinha, 25, ambaye analengwa na Arsenal.

Leeds wanamthamini Raphinha kwa pauni milioni 65 huku Tottenham, Chelsea na Barcelona pia wakimtaka. Nice wanalenga mkataba wa mkopo na mlinda lango wa Chelsea Mhispania Kepa Arrizabalaga, 27.

Mshambulizi wa Chelsea na Albania Armando Broja, 20, atakuwa tayari kuhamia West Ham kwa dau la pauni milioni 25 linalokuja.

Chelsea inamngoja mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Inter Milan kabla ya kushughulikia nia yao ya kumnunua fowadi wa Manchester City na Uingereza Raheem Sterling, 27.

Kiungo wa kati wa Reims na Zimbabwe Marshall Munetsi, 26 anaweza kuletwa na Brighton kuchukua nafasi ya Yves Bissouma, kiungo wa kati wa Mali aliihama klabu hiyo na kuelekea Tottenham.

Kipa wa Ujerumani Loris Karius, 29, yuko tayari kwa changamoto mpya anapotafuta klabu mpya ambayo huenda kuondoka kwake Liverpool kukiribia.

Mshambulizi wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 26, ana nia zaidi ya kujiunga na Liverpool badala ya AC Milan.

Mshambulizi wa Brazil Vinicius Jr, 21, anasema ataweka mustakabali wake Real Madrid licha ya Paris Saint-Germain kumtaka.