14 May 2022 / 37 views
Sanamu ya Aguero yazinduliwa

Mkongwe wa klabu ya Manchester City, Sergio Aguero  amesema kuwa sanamu lake jina ni alama ya kumbukumbu ya miaka 10 toka washinde ubingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza ni kumbukumbu muhimu katika maisha yake.

Sanamu hilo limezinduliwa kwenye uwanja wa Etihad ambalo linaonesha jinsi Aguero akishangilia goli lililoipa ushindi dakika za mwisho msimu wa mwaka 2011-12.

Aguero amesema kuwa kumbukumbu hiyo imebadilisha maisha yake binafsi pamoja na mabadiliko ya klabu kuanzia timu hiyo ikaanza kuonekana kubwa barani Ulaya.

Sanamu hilo limetengenezwa na Sculptor Andy Scott ambalo limezinduliwa leo siku ya Ijumaa uwanjani hapo huku mchezaji huyo akihudhuriwa uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa City, Khaldoon al-Mubarak amesema kuwa goli la Aguero dhidi ya QPR mwaka 2012 liliifanya Manchester United kukosa ubinwa na kubadilisha kila kitu kwenye klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo ameshinda mataji 15 ndani ya miaka 10 akiwa na Manchester City na kufanikiwa kuwa mfungaji wan ne katika historia ya ligi ya Uingereza akishinda magoli 184 katika mechi 275.

Aguero aliachana na City msimu uliopita na kujinga na Barcelona kabla kustaafu kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo.