14 May 2022 / 54 views
Coutinho amalizana na Aston Villa

Klabu ya Aston Villa imekamilisha usajili wa mchezaji wa zamani wa Liverpool, Phileppe Coutinho akitokea klabu ya Barcelona.

Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Villa Park kwa mkopo January  huku kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja.

Sasa amesaini mkataba mpaka mpaka msimu wa mwaka 2026 kwa euro milioni 20 na amekubali kupunguza mshahara wake.

"Huu ni usajili bora kwa Aston Villa alisema kocha wa Aston Villa "Phil ni mchezaji wa kisasa na matokeo yake yameonekana toka ajiunge mwezi Januari mwaka huu.

"Kwa jinsi anavyojiendesha ndani na nje ya uwanja, yeye pia ni mfano muhimu kwa wachezaji wetu wachanga ambao wanaweza kufaidika tu na uzoefu wake.

"Tunapotarajia kujiandaa kwa msimu ujao, ni jambo la kushangaza kufanya kazi katika klabu ambayo inatekeleza shughuli zake kwa uthabiti na kwa urahisi."

Coutinho amefunga mabao manne na kutoa pasi tatu za mabao akiwa Villa, ingawa hakuna hata moja kati ya hizo iliyopatikana katika mechi nane zilizopita.

Alijiunga na Barcelona kwa uhamisho wa pauni milioni 142 kutoka Liverpool Januari 2018 na alikuwa amebakisha miezi 12 kwenye mkataba wake.

Gerrard, ambaye alikuwa nahodha wa Coutinho huko Liverpool, aliweka wazi baada ya ushindi wa 3-1 Jumamosi dhidi ya Burnley kwamba alitaka kumsajili Coutinho kabisa.

Coutinho alifunga mabao 54 katika mechi 201 akiwa na Liverpool, ambayo alijiunga nayo kwa uhamisho wa pauni milioni 8.5 kutoka Inter Milan Januari 2013.