14 May 2022 / 55 views
Tetesi za usajili Ulaya

Bayern Munich wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua mchezaji wa United ambaye atakuwa huru hivi karibuni Paul Pogba, huku Juventus, Paris St-Germain, Real Madrid na Manchester City wakiwa tayari kuwinda saini ya kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29.

Newcastle itawasilisha ombi la kumsajili katika msimu wa joto mshambuliaji wa Everton na Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 25, kama lengo la kipaumbele chake.

The Magpies wamekuwa na nia ya muda mrefu kwa mchezaji huyo, kama ilivyo kwa Arsenal.

Robert Lewandowski, 33, hatasaini mkataba mpya Bayern Munich, na mshambuliaji huyo wa Poland anaweza kuuzwa kwa Barcelona msimu huu wa joto kabla ya kuingia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake.

Chelsea wanataka kukamilisha usajili wa mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, mapema katika dirisha la kiangazi.

Meneja Pep Guardiola atamaliza mkataba wake na Manchester City, ambao unamalizika 2023, badala ya kusaini nyongeza msimu huu wa joto.

Mhispania huyo atafanya uamuzi wa "dakika ya mwisho" kuhusu kuongeza muda.

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 27, anatarajia kujiunga na moja ya klabu maarufu barani Ulaya iwapo ataondoka Etihad msimu wa joto, licha ya kumtaka Arsenal na Tottenham.