14 May 2022 / 57 views
Mane kutua Bayern Munich

Klabu ya Bayern Munich inavutia na kiungo wa Liverpool, Sadio Mane na wana nia ya kumsajili msimu huu wa kiangazi.

Ila hakuna mazungumzo maalum kati ya klabu hizo mbili, Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich, Hasan Salihamidzic amekutana na wakala wa mchezaji huyo mwisho wa wiki.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal bado ana mkataba mpaka msimu wa mwaka 2023 lakini mazungumzo yanawezekana yakawa magumu kufikika, Mane hana furaha na mkataba mpya wa Mohamed Salah ambao utamfanya awe mchezaji mwenye thamani ndani ya Anfield.

Mane amecheza mechi 47 kwenye michuano yote na ameshinda jumla ya magoli 21 msimu huu ndani ya klanu ya Liverpool.

Mshambuliaji huyo hapo awali alihusishwa kuondoka ndani ya Anfield ambapo alitakiwa kujiunga na Real Madrid hapo awali.

Baada ya sare 2-2 dhidi ya Stuttgart kwenye mechi ya ligi ya Bundersliga, Salihamidzic amesema kuwa kuna jina kubwa la mchezaji mwingine atajiunga na klabu hiyo msimu huu.