12 May 2022 / 57 views
Gurdiola: Kila mtu anashabikia Liverpool

Kocha Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa kila mmoja anaisapoti Liverpool ndani ya Uingereza baada ya timu yake kuongoza ligi kwa tofauti ya alama tatu.

Manchester City walishinda 5-0 dhidi ya Newcastle United siku ya Jumapili baada ya Liverpool kutoka 1-1 na Tottenham kwenye mechi ya ligi kuu soka nchini Uingereza.

Manchester City imetolewa kwenye ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali dhidi ya Real Madrid wiki iliyopita.

"Bila shaka kwasababu Liverpool ana historia nzuri kwenye michuano ya Ulaya lakini siyo kwenye ligi ya Uingereza kwasababu wameshinda ubingwa mara moja ndani ya miaka 30 lakini siyo tatizo kabisa.

Guardiola anatafuta taji la nne la EPL ndani ya miaka yake mitano toka aanze kuifundisha klabu hiyo akitokea Bayern Munich, huku Kloop akishinda taji hilo msimu wa 2019-20.

"Liverpool wako pamoja na [Manchester] United kama timu muhimu zaidi katika suala la mataji, urithi, historia, mchezo wa kuigiza kwa mambo mengi," alisema Guardiola.

"Lakini tumekuwepo tangu miaka 11 au 12 iliyopita. Najua wakati mwingine tunakosa raha, lakini sijali kama watu wanataka Liverpool ishinde zaidi yetu. Sio suala."