12 May 2022 / 84 views
Haaland mbioni kutua Man City

Mshambuliaji wa Poland, Erling Haaland yupo mbioni kujiunga na Manchester City akitokea from Borussia Dortmund ndani ya wiki hii.

Inasemekana kuwa dau la mchezaji huyo litakuwa Euro milioni 63 ambapo mchezaji huyo amekubali dau hilo na uhenda ndani ya wiki hii atatangazwa kuwa mchezaji wa Manchester City.

Wakala wa wachezaji Mino Raiola alihusika katika mazungumzo ya uhamisho wa mchezaji huyo kabla ya kufariki.

Japokuwa Manchester City inakaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza wamecheza bila ya kuwa na mshambuliaji.

Manchester City wamejaribu sana kumpata mchezaji Harry Kane msimu uliopita lakini mwenyekiti wa Tottenham Dany Levy kukataa kumuuza mchezaji huo.

Kane amebakiwa na miaka miwili kwenye mkataba wake, ila kwa Haaland imekuwa ni raisi sana kwa mchezaji huyo kutua Manchester City.

Mchezaji huyo ameshinda magoli 92 katika mechi alizocheza katika klabu za Molde, Red Bull Salzburg na Borussia Dortmund.

Mwaka jana amekuwa mchezaji kijana kufikisha jumla ya magoli 20 katika ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na umri wa miaka 20.