14 May 2022 / 54 views
Tetesi za usajili Ulaya

Klabu ya Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 27 kama Manchester City itakubali kumuuza mwishoni mwa msimu huu, ambapo mkataba wake utakua umesalia mwaka mmoja.

The Gunners pia wameanza mazungumzo na kiungo wake wa Misri, 29 Mohamed Elneny, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu.

Bayern Munich wanapanga kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 30, huku magwiji hao wa Ujerumani wakiwa tayari wamewasiliana na wakala wa mchezaji huyo.

Nyota wa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain, 28, anahofu na mustakabali wake Anfield future, ambapo hajaambiwa lolote kuhusu mkataba mpya na hajacheza mchezo wowote tangu Machi 20. Mkataba wa kiungo huyo muingereza unamalizika msimu ujao.

Kiungo mfaransa Paul Pogba, 29 ambaye mkataba wake na Manchester United unamalizika mwishoni mwa msimu, ameiambia Manchester City kwamba hana nia ya kujiunga nayo ikielezwa kwamba nyota huyo ataelekea klabu nyingine tofauti.

Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel anatarajiwa kuelezwa kwamba ataungwa mkono na wamiliki wapya wa klabu hiyo.

Meneja wa Newcastle United Eddie Howe atasikiliza ofa za wachezaji karibu 10 katika dirisha lijalo la usajili akiwemo nahodha Jamaal Lascelles, 28 huku mlinzi huyo muingereza akikosa namba kwenye kikosi hicho.

Mlinzi wa Chelsea Jake Clarke-Salter, 24, ianasakwa na Leeds United na PSV Eindhoven baada ya kuonyesha kiwango bora akiwa kwa mkopo na klabu ya Championship Coventry City. Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 anakaribia kumaliza mkataba wake Stamford Bridge.

Meneja wa Barcelona Xavi anasema hali yao kifedha inawaondoa katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, ambaye anajiandaa kutua Manchester City kutoka Borussia Dortmund.