30 Nov 2021 / 43 views
Barcelona wamtaka Martial

Klabu ya Barcelona pia wanavutiwa na mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial, 25.

Barcelona wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na Uhispania Ferran Torres, 21.Viongozi wa Barcelona wamezungumza na wawakilishi wa Torres katika sherehe za Ballon d'Or.

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, hivi majuzi alizungumza na rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi lakini klabu hiyo ya Ufaransa inasisitiza kuwa haikuwa kitu zaidi ya kukutana tu.

Leeds wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid Mariano Diaz, 28, ambaye ana mechi moja katika Jamhuri ya Dominika.

Malang Sarr wa Chelsea, 22, analengwa na Inter Milan. Beki huyo wa Ufaransa amecheza mechi tatu pekee tangu ajiunge nayo mwaka 2020.(Sport Mediaset via Sun)

Newcastle wanampango wa kutumia ''kiasi kikubwa cha fedha'' kumnasa kiungo wa kati wa Inter Milan Marcelo Brozovic. Flamengo wanafikiria kumnunua mlinzi wa kati wa Arsenal na Uhispania Pablo Mari Januari 28.

Espirito Santo anataka kurejea haraka kwenye uongozi kufuatia kufukuzwa kwake na Tottenham lakini kuna uwezekano wa klabu ya Ligi ya Premia kuliko kuripotiwa kuhamia Ligue 1.