30 Nov 2021 / 47 views
Messi ashinda Ballon d'or

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi ameibuka mshindi wa taji la Ballon d'Or - linalokabidhiwa mchezaji bora wa soka wa mwaka kwa mara ya saba.

Messi aliisaidia nchi yake kushinda taji la Copa America likiwa ndio taji lake la kwanza la kimataifa , na amefunga magoli 40 mwaka 2021 - 28 akiifungia Barcelona , manne akiifungia PSG na manane akiifungia Argentina.

Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski alikuwa wa pili , huku kiungo wa kati wa Chelsea na Itali Jorginho akiwa wa tatu , naye mshambuliaji wa Real Madrid na Ufaransa Karim Benzema akiwa katika nafasi ya nne.

Taji hilo hupigiwa kura na waandishi 180 kutoka kote duniani , ijapokuwa hakukuwa na taji lililotolewa mwaka 2020 kutokana na mlipuko wa jangwa la corona.

Messi na Christiano Ronaldo walifanikiwa kushinda taji hilo mara tano kila mwaka kuanzia 2008, 2019 isipokuwa 2018 wakati kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric alipotawazwa kuwa mshindi

Messi alikuwa tayari ashaibuka mshindi mara nyingi zaidi ya mchezaji mwengine yeyote baada ya kushinda mwaka 2009, 2010, 2012, 2015 na 2019.

"Ni furaha isio na kifani kuwa hapa tena ," alisema katika sherehe hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Paris wa Theatre du Chatelet.

Lewandowski alifunga magoli 53 katika mashindano yote 2021 akiichezea Bayern na alituzwa tuzo la mshambuliaji wa mwaka , tuzo mpya ambayo ilitangazwa saa chache kabla ya sherehe hiyo kuanza.

Kipa wa Paris St-Germain Gianluigi Donnarumma, ambaye aliisaidia Itali kushinda kombe la Euro 2020, alishinda taji la Yashin Trophy kwa kuwa kipa bora , huku klabu ya Chelsea ilioshinda taji la klabu bingwa Ulaya ikishinda tuzo ya klabu bora ya mwaka.

Kiungo wa kati wa Barcelona Pedri, 19, alishinda tuzo ya Kopa Trophy kwa kuwa mchezaji bora mwenye umri mdogo wa miaka ya chini miaka 21 , huku mchezaji wa England Jude Bellingham , Mason Greenwood na Bukayo Saka wakichukua nafasi ya pili ya tano na ya sita mtawalia.

Chelsea ilikuwa na wachezaji watano , huku mchezaji aliyeibuka katika nafasi ya tatu Jorginho akijiunga na N'Golo Kante katika nafasi ya tano Romelu Lukaku katika nafasi 12, Mason Mount katika nafasi 19 na Cesar Azpilicueta, akiwa katika nafasi ya 29.