29 Nov 2021 / 52 views
Roma yaendeleza vipigo Seria A

Fowadi wa Uingereza Tammy Abraham alifunga bao la ushindi kwa Roma dhidi ya Torino huku kikosi cha Jose Mourinho kikipata ushindi wa tatu mfululizo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga bao lake la tano katika mechi nne za mashindano yote katika kipindi cha kwanza.

Hapo awali, Abraham alidhani amepata penalti lakini uamuzi huo ulibatilishwa baada ya kuamuliwa kuwa ameotea na mwamuzi msaidizi wa video.

Roma iko katika nafasi ya tano kwenye Serie A, pointi tatu nyuma ya Atalanta iliyo nafasi ya nne.

Bao la Abraham linafikisha jumla ya mabao yake kwa msimu huu hadi tisa katika mashindano yote.