13 Oct 2021 / 55 views
Ubora wa Pogba ndani ya Man United

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba mpaka sasa ndani ya Manchester United ambapo aliibukia hapo 2016 akitokea Klabu ya Juventus amecheza jumla ya mechi 144 za ushindani.

Alipokuwa Juventus msimu wa 2012/2016 aliweza kucheza jumla ya mechi 124 na alitupia mabao 28 kama umri wake wa sasa.

Weka kando ishu za Juventus sasa tunarudi katika Klabu ya Manchester United ambapo yupo kwa sasa huku dili lake nalo likizidi kuyeyuka taratibu na anatajwa kuingia kwenye rada za Real Madrid.

Katika mechi 144 ambazo amecheza ametupia pia mabao 28 na pasi alizotoa ni 36 ametengeneza nafasi za wazi 27 pia amekosa nafasi za wazi kufunga 28.

Hivyo kama angefanikiwa kufunga katika kila nafasi ambazo alizipata hizo za wazi mwamba angekuwa ametupia jumla ya mabao 56 kibindoni ila hakuwa na bahati mabao yake yatabaki kuwa 28.

Rekodi zinaonyesha kwamba amepiga jumla ya pasi 8,785 ikiwa ni wastani wa pasi 61 katika kila mechi na hizi ni rekodi za Premier League pekee.