13 Oct 2021 / 54 views
Tetesi za usajili Ulaya

Wakala wa Erling Braut Haaland, Mino Raiola anatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester City kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mshambuliaji huyo wa miaka 21 wa Borussia Dortmund na Norway msimu wa joto.

Mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, anataka kuhakikishiwa kwamba ni sehemu muhimu ya mipango ya Pep Guardiola kabla ya kuanza tena mazungumzo ya mkataba na Manchester City.

Liverpool wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa England Alex Oxlade-Chamberlain, 28, - lakini kwa bei stahiki - huku klabu yake ya zamani ya Arsenal ikimtaka.

The Reds pia wameanza majadiliano ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Mfaransa Ousmane Dembele, 24, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto.

Kiungo wa kati wa England Phil Foden, 21, anakaribia kutia saini mkataba mpya Manchester City. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2024.

Manchester United wameungana na Chelsea na Juventus katikambio za kumsaka kiungo wakati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni.

Mlinzi wa Barcelona Clement Lenglet, 26, huenda akawa wa kwanza kuwasili Newcastle baada ya klabu hiyo kununuliwa hivi kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa akisemekana kuwa mchezaji klabu hiyo inamtaka.

Wachezaji wa Southampton wanatarajia kocha wao Ralph Hasenhuttl, 54, atafutwa katika wiki chache zijazo hata. Kabla ya klabu hiyo kushinda taji ya Ligi ya Primia msimu huu.

Mchezaji wa Uhispania Hector Bellerin, 26, amedokeza kwamba hana nia ya kurejea Arsenal mkataba wake wa mkopo wa msimu mzima Real Betis utakapokamilika.