04 May 2021 / 175 views
Mbappe hati hati kukosa nusu fainali

Kocha wa PSG, Mauricio Pochettino amesema suala la Kylian Mbappe kucheza ama kutocheza mchezo wa leo dhidi ya Manchester City kwenye nusu fainali ya mkondo wa pili bado halijafanyiwa maamuzi.

Pochettino amesema, “ Tunahitaji kumfanyia vipimo Mbappe. Ataendelea na mazoezi binafsi na tutaangalia kama anaweza kuwa sehemu ya timu. Kuna muda umesalia na tutaamua kama atakuwepo”.

Mbappe amejipambanua kama mchezaji tegemezi kwenye safu ya ushambuliaji ya PSG, kwani amefanikiwa kufunga mabao 8 na kutengeneza 3 kwenye michezo 10 aliyocheza kwenye michuano ya klabu bhingwa Ulaya, utofauti wa mabao 2 na kinara wa ufungaji Braut Haaland.

Kwa upande wa michuano yote, Mbappe ameshaifungia PSG mabao 37 na kutengeneza mengine 10 sawa na kuhusika kwenye mabao 47 katika michezo 43 aliyoichezea klabu yake hiyo ya matajiri wa jiji la Paris nchini Ufaransa kwenye michuano yote.

Kuzungumzia namna mchezo utakavyo kuwa na maandalizi yake, Pochettino amesema, “Tunahitaji kuwa tayari kuteseka kwenye nyakati fukani kimchezo, na tukipata nafasi tunapaswa kuwa watumiaji wazuri wa nafasi na kuchangamka”

PSG wanatazamiwa kumkosa kiugo wake mkabaji, Idriss Gueye Gana ambaye anakosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja kufuatia kadi nyekundu aliyooneshwa kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

Manchester City hawana wachezaji wenye majeraha isipokuwa mlinzi chipukizi, Erick Garcia ana sumbuliwa na ugonjwa wa Malaria akiwa ndiyo mchezaji pekee atakayekosekana.

PSG ataingia na kumbukumbu yakupoteza mchezo wake wa mwisho kwenye dimba la Etihad, kwa kufungwa bao 1-0 na kuondoshwa kwenye hatua ya robo fainali Aprili 2016 kwa bao pekee la Kevin De Bruyne.