04 May 2021 / 41 views
Vidal atwaa mataji tisa misimu kumi

Baada ya kutwaa taji la ubingwa wa Serie A msimu huu kiungo Inter Milan, Arturo Vidal amefanikiwa kutwaa mataji tisa ya ligi tofauti ndani ya miaka 10.

Vidal amefanikiwa kutwaa mataji hayo akiwa na Juventus ambapo alishinda manne ya Serie A, 2012 mpaka 2015.

Ndani ya Bundesliga na kikosi cha Bayern Munich alibeba taji la ligi hiyo mara tatu msimu wa 2015/16, 2016/17 na 2017/18.

Msimu wa 2018/19 alitwaa taji la La Liga akiwa na Barcelona ambapo aliondoka msimu uliopita na kutua Inter Milan.

Mchezaji huyo amecheza katika klabu kubwa barani Ulaya kama vile, Juventus, Bayern Munich, Barcelona pamoja na Inter Milan.

Katika miaka hiyo 10 Vidal hakushinda taji msimu wa 2019/10 akiwa ndani ya Barcelona na ni msimu pekee ambao hakutoka na taji la ligi.