04 May 2021 / 35 views
Gurdiola awatahadharisha wachezaji wake

Kocha wa Manchester City, Pepe Gurdiol amesema kuwa mchezo wake wa leo dhidi ya PSG hautakuwa mwepesi licha ya ule wa awali kuweza kushinda kwa mabao 2-1.

Mchezo wa leo ni wa Champions League ikiwa ni nusu fainali ya pili na mshindi wa jumla atatinga fainali ambapo PSG inakumbuka kwamba ilipoteza mchezo wa nusu fainali ya kwanza ilipokuwa nyumbani. 

Imekuwa inaonesha kwamba City ina nafasi ya kutinga hatua ya fainali kutokana na ubora wa wachezaji wake pamoja na mbinu za Guardiola akiwa ndani ya Uwanja wa Etihad jambo ambalo ameliweka wazi kwamba sio jepesi.

Vinara hao wa Ligi Kuu England wanapewa pia nafasi ya kutwaa taji hilo ambalo lipo mikononi mwa Liverpool inayonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp ambaye hana mwendo mzuri kwa sasa katika kutetea taji hilo kutokana na kuandamwa na wachezaji wake wengi ambao wanasumbuliwa na majeraha.

Kocha Mkuu wa PSG, Mauricio Pochettino amesema kuwa utakuwa ni mchezo mgumu kwa pande zote mbili bila kujali nani yupo nyumbani kutokana na ubora wa wachezaji waliopo.

"Hautakuwa mchezo mwepesi kwa timu zote mbili hasa ukizingatia kwamba kila upande una wachezaji wazuri, tupo tayari kwa ajili ya ushindani na tutapambana kufanya vizuri,".

 Guardiola amesema kuwa itakuwa ngumu kwake kuweza kulinda kiwango cha wachezaji wake mbele ya PSG inayonolewa na Mauriccio Pochetino.

"Haiwezekani kuweza kuendelea kuwa kwenye kiwango bora kama awali na huwezi kutabiri kuhusu mchezo wetu mbele ya PSG nina amini kwamba utakuwa mchezo mgumu na jambo lolote linaweza kutokea ndani ya dakika 90.

"Sio tofauti na wakati ule ambao tumefanya vizuri ila kuna kitu cha kipekee ambacho kitafanyika, kiuhalisia ni ngumu  timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu England ubora wake ni sawa na  ule wa PSG hivyo huwezi kutabiri,".