04 May 2021 / 31 views
Pogba avutiwa na Casemiro na Kante

Kiungo wa Manchester United Paulo Pogba amewataja N'golo Kante na Casemiro kuwa ndiyo wachezaji wanaompa upinzani mkubwa wakutanapo uwanjani.

Alipoulizwa juu ya wapinzani wake wakubwa uwanjani, hakusita kuwataja N'golo Kante wa Chelsea na Casemiro wa Real Madrid ambao jumatano hii watakutana dimbani kwenye nusu fainali ya pili ya klabu bingwa Ulaya

''Kwa upande wangu niwe mkweli tu, N'golo Kante ni mpinzani anayenisumbua sana nikutanapo naye anacheza kwa kuhamahama maeneo ndani ya uwanja ni ngumu sana kumkaba mchezaji wa aina hii'' alisema Pogba

''Mwingine ni Casemiro, huyu jamaa ni hatari sana anajua kucheza mipira ya aina zote, ana nguvu na maarifa makubwa sana awapo uwanjani mwisho wa siku amejengwa na jihadi ya hali ya juu, kifupi ni mshindani halisi'' aliongeza Pogba

Kiungo huyu aliyosajiliwa 2016/17 kwa dau kubwa na United akitokea Juventus ameiongoza vyema timu yake katika ushindi wa 6-2 dhidi ya AS Roma walioupata wiki iliyopita wanajiandaa na mchezo wa marudiano Alhamis hii.