04 May 2021 / 38 views
Tetesi za usajili Ulaya

Leicester City na Everton ni miongoni mwa vilabu vinavyojiandaa na mchakato wa kumnasa mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, 25.

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy atampa meneja ajaye wa klabu nafasi ya kumsainisha tena mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, kwa mkopo kutoka Real Madrid kwa msimu wa 2021-22.

Borrusia Dortmund itamuacha mchezaji wa kimataifa wa England Jadon Sancho kuondoka katika klabu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 87, baada ya hapo awali kutaka kiasi cha pauni milioni 100 kwa ajili ya kiungo huyo wa kati.

Mchezaji huyo, 21 amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Liverpool na Manchester United.

Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke amerejelea msimamo wa klabu kwamba mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United,Liverpool , Manchester City , Chelsea, Barcelona na Real Madrid- hatauzwa msimu wa joto.

Newcastle United na klabu ya Italia, Atlanta zimeonesha nia hasa na mchezaji wa nafasi ya ulinzi ya Vitesse Arnhem Danilho Doekhi, 22, ambaye pia anahusishwa na taarifa za kutolewa macho na Norwich City, Fulham na mabingwa wa ligi ya primia ya Uskoti, Rangers.

Wakala wa Robert Lewandowski Pini Zahavi anajiandaa kutia msukumo kwa Bayern Munich kumpa mkataba mpya mshambuliaji wa Poland au kumuuza katika klabu ambayo itaweza kummudu.

Watford wamefanya mawasiliano na Inter Milan na mlinzi wa England Ashley Young, 35, kuhusu kurejea kwenye klabu hiyo, ambako alianza kazi yake.

Familia ya Glazer inaweza kushawishiwa kuiuza Manchester United, lakini kiasi cha pauni bilioni 4 kinaweza kujaribu kuwashawishi.

Klabu ya Ufaransa Nice imeendelea kuonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati Jesse Lingard baada ya kumkosa alipojiunga kwa mkopo West Ham akitokea Manchester United mwezi Januari.

Newcastle United ina nia ya kumuongezea mkataba mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Uswisi Fabian Schar,29, kabla ya michuano ya mabingwa Ulaya.