03 May 2021 / 37 views
PSG wataka saini ya Messi

Klabu ya Paris Saint Germain imeelezwa kwa sasa ipo kumshawishi staa wa Barcelona, Lionel Messi kujiunga na klabu hiyo, kumpa ofa ya miaka miwili.

Messi kwa sasa anaweza kuongea na timu yoyote kwani mkataba wake umesalia wa mwezi mmoja ndani ya Barcelona. Ripoti zinaeleza mpaka sasa haijafahamika kama Messi atasalia kikosini hapo au ataondoka.

Taarifa zainaeleza kuwa PSG imetoa ofa ya miaka miwili mezani kwa ajili ya staa huyo kutua kikosini hapo.Ripoti zinaeleza kuwa sababu ya PSG kutaka kumchukua Messi ni kuona staa huyo anafanikiwa kwa mara nyingine kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na uzi wao.

Imeelezwa kuwa sasa hakuna kipya ndani ya Barcelona kwani kinachosubiriwa ni jibu la Messi kama anabaki au anaondoka.

PSG wao wapo tayari kumsajili staa huyo na kuongeza nguvu ndani ya kikosi chao ambacho kina vijana kibao wenye ubora.

Kwa upande mwingine, taarifa zinaeleza kuwa Rais wa Barcelona Joan Laporta bado anapambana kuhakikisha Messi anaendelea kusalia ndani ya Barcelona.