08 Apr 2021 / 38 views
Rashford kuwakabili Granada leo

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford atawakabili Granada katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Europa Leo.

Rashford alifunga katika ushindi wa Jumapili wa 2-1 dhidi ya Brighton lakini akaondolewa baada ya kupata majeraha kwenye mechi hiyo.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha mchezaji huyo wa kimataifa wa England yuko fiti kusafiri kwenda Uhispania.

"Tunapaswa tu kufanya uamuzi ikiwa ataanza au yuko kwenye benchi," alisema. "Sidhani atakuwa mtu wa dakika 90."

Juan Mata amejumuishwa katika kikosi cha wasafiri pamoja na Anthony Elanga wa miaka 18. Anthony Martial anawekwa pembeni na jeraha la goti wakati Eric Bailly anakosa baada ya kukutwa na virusi vya Corona.