08 Apr 2021 / 150 views
Tetesi za usajili Ulaya

West Ham itafanya vyovyote vile ili kumnasa kiungo wa kati Jesse Lingard, 28, anayekipiga Manchester United.

Thamani ya Lingard kwa mujibu wa Manchester United ni pauni milioni 30. Arsenal imerejesha nia yao tena kwa mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha,28.

Manchester City wanalenga kukubaliana kuingia mkataba mpya nawashambuliaji wa England Phil Foden,20, na Raheem Sterling,26, kabla ya mwishoni mwa msimu, baada ya kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne,29, kuongeza mkataba wake wa mpaka mwaka 2025.

Manchester City haitamfuatilia mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi mpaka mchezaji huyo, 33, atakapoweka wazi kuwa anataka kuondoka Barcelona.

Chelsea wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86.3 kwa ajili ya mshambuliaji Mbelgiji anayecheza katika klabu ya Inter Milan Romelu Lukaku, 27, endapo the Blues watashindwa kumsajili mshambuliaji Erling Braut Haaland,20, wa Borussia Dortmund.

Tottenham watajaribu kumsajili mlinzi wa kati wa Southampton Jannik Vestergaard,28, mwenya thamani ya pauni milioni 18, baada ya dirisha la usajili kufunguliwa.

Liverpool wameiambia RB Leipzig kuwa hawatamsajili mlinzi wa kati, Mfaransa Ibrahima Konate,21,

Reds watakabiliwa na ushindani wa Chelsea katika kumnasa kiungo wa kati wa Ajax Ryan Gravenberch ambaye anatazamwa kuwa mbadala wa Georginio Wijnaldum.

Kocha wa zamani wa Bournemouth anamtaka mshambuliaji wa Everton Josh King,29, kuwa mchezaji wa kwanza kumsajili akiwa kocha wa Celtic.