08 Apr 2021 / 38 views
Varane akutwa na virusi vya Corona

Beki wa Real Madrid, Raphael Varane amepimwa na kukutwa na maambukizi ya Covid-19 baada ya kuonesha dalili na kuamua kupimwa.

Klabu ya Uhispania ilisema ikimwondoa katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool Leo.

Mabingwa mara 13 wa ligi ya mabingwa watamkosa beki huyo chaguo la kwanza kwa mchezo dhidi ya Liverpool labda mchezo wa pili huko Anfield mnamo Aprili 14.

Zinedine Zidane yuko mbioni kumuanzisha Mhispania Nacho Fernandez pamoja na Mbrazil Eder Militao katikati safu ya ulinzi kwenye mchezo wa kwanza, marudio ya fainali ya Ligi ya Mabingwa 2018 ambayo Real ilishinda 3-1.