08 Apr 2021 / 26 views
Martial kukosi mechi za mwisho za msimu huu

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Anthony Martial huenda akakosa michezo yote ya msimu huu mwaka 2020-21 baada ya vipimo kuonesha kuwa ameathiri pakubwa kwenye goti lake na atakuwa nje kwa majuma mengi zaidi.

Martial alipata majeraha hayo akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa kwenye mchezo dhidi ya Kazhakstan ambapo alifanikiwa kutengeneza bao la kwanza kabla ya kufanyiwa mabadiliko baada ya maumivu hayo.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjear amesema wanahitaji kufanyakazi ya ziada kuziba pengo la mchezaji huyo ambaye pia nafasi yake ya kushiriki michuano ya mataifa ya Ulaya UEFA EURO ya mwaka 2020 kama bado atakuwa hajapata unafuu hadi mwishoni mwa mwezi mei 2021.

Martial ameifungia klabu yake mabao 7 na kutengeneza mengine 8 kwenye michezo 36 aliyoichezea tokea kuanza kwa msimu huu.