06 Mar 2021 / 42 views
Solskjaer akiri timu yake kushuka

Kocha wa Manchester United, OLE Gunnar Solskjaer amekiri kuwa anapata hofu kuhusu kushuka kwa kiwango cha timu yake na kushindwa kufunga mabao baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Crystal Palace.

Manchester United sasa imecheza mechi tatu mfululizo bila kupata bao, mbili zikiwa ni za Premier na moja ya Ligi ya Europa dhidi ya Real Sociedad.

Kocha huyo wa Manchester United, amesema: “Wakati mwingine haufikii kile kiwango ulichonacho na ulichokuwa nacho kwa miezi mingi sana. Inaleta hofu bila shaka lakini najua kwamba vijana wanajitoa kwa kila kitu.“

Tunacheza kila baada ya siku tatu na najua wanajitoa kwa kila kitu walichonacho. Ninafurahishwa na hilo.” Dean Henderson alidaka badala ya David de Gea ambaye alitajwa hakuwepo kutokana na sababu binafsi, na Dean hakuruhusu bao huku akiiokoa United kufungwa bao dakika ya mwisho.

Alipoulizwa kama De Gea atakosekana katika dabi ya Jumapili dhidi ya Manchester City, Solskjaer aliongeza: “Siwezi kuzungumza kuhusu David. Ni suala binafsi. Dean yupo tayari kama akihitajika.”.