08 Mar 2021 / 65 views
Arsenal kufanya usajili mpya

Arsenal ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazoangalia uwezekano wa kumhamisha mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya RB Leipzig Mfaransa Ibrahima Konate mweye umri wa miaka 21.

Konate ni mmoja kati ya wachezaji sita ambao Gunners wanashugulika kuwapata, huku klabu hiyo pia ikiwa tayari kumuuza mshambuliaji wa Ufarnsa Alexandre Lacazette, 29, kwa bei inayofaa.

Kiungo wa kati wa Manchester United Mreno Bruno Fernandes, 26,yuko tayari kusaini mkataba mpya ambao utaongeza mshahara wake mara dufu na kuweza kupata malipo ya takriban pauni 200,000 kwa wiki.

Mlinzi wa Misri Ahmed Elmohamady, 33, ataondoka Aston Villa kwa mkataba usio na malipo msimu huu huku klabu hiyo ikiwa haina mipango ya kumpatia mkataba mpya.

Napoli wamepunguza kiwango cha pesa walizokuwa wanadai kwa ajili ya kumuuza Kalidou Koulibaly hadi kufikia kiwango cha euro milioni 45 (£38.7m), huku Bayern Munich wakiaminiwa kuwa mbele ya Liverpool na Manchester United katika mbio za kusaini mkataba na mlinzi huyo kutoka Senegal mwenye umri wa miaka 21.

Leicester City wamefufua haja yao kwa mchezaji ambaye wamekuwa wakimtaka kwa muda mrefu Ismail Jakobs, mwenye umri wa miaka 21, lakini the Foxes wanakabiliwa na ushindani kutoka Brighton ambao pia wanamfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa kimataifa kutoka klabu ya Ujerumani ya Cologne.

Manchester United wanatafuta klabu mbadala kwa ajili ya kiungo wa kati Andreas Pereira, 25, msimu huu kwasababu Lazio wanatarajiwa kukubali hilo na kubadilisha makataba wa Mbrazili huo kutoka mkataba wa mkopo na kusaini mkataba wa kudumu nae.

Shinikizo la kifedha linaweza kuilazimisha klabu ya Valencia kumuuza mshambuliaji wa Ureno Goncalo Guedes, 24, ambaye analengwa na West Ham katika msimu ujao.