06 Mar 2021 / 174 views
Tetesi za usajili Ulaya

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland,20, anaenyatiwa na Chelsea- amesema kuna klabu sita ambazo huenda akajiunga nazo, Liverpool, Manchester United na Manchester City ndizo klabu za Ligi ya Primia anazopigiwa upatu.

Dortmund ina mpango wa kuwa na Haaland baada ya msimu huu, kulingana na mkuu wa kikosi cha kwanza cha soka, Sebastian Kehl.

Arsenal inatathmini uwezekano wa kumnunua mlinzi wa Brighton na England Tariq Lamptey, 20, na beki wa Norwich Muingereza Max Aarons, 21, kuchukua nafasi ya Hector Bellerin, 25, ambaye amehusishwa na tetesi za kujiunga na Paris St-Germain.

Chelsea itatia kibindoni asilimia isiyojulikana ya ada itakayopokewa na Brighton wakimuuza Lamptey baada klabu hizo mbili kukubaliana katika mpango ambao ulimwezesha mlinzi huyo kuondoka Stamford Bridge na kutua Seagulls Januari 2020.

Mgombea uraisi wa Barcelona Joan Laporta anataka mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, kujiunga na klabu hiyo msimu huu.

Mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta amesema "umakini kabisa" kuongoza Arsenal licha ya madai yanayomhusisha Barcelona - lakini mazungumzo ya mkataba mpya utakaomwezesha kusalia Emirates hayajaanza.

Arteta anasema mazungumzo kuhusu kandarasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette,29, ambaye mkataba wake wa sasa na Arsenal unaendelea hadi 2023, yataanza hivi "karibuni".

Winga wa zamani wa England Ashley Young, 35, anamatumaini ya kunyakua taji la Serie, Inter Milan kabla ya kurejea klabu katika yake ya kwanza ya Watford kwa mkataba wa bila malipo msimu huu.

Meneja Jurgen Klopp amekiri kuwa Liverpool itakuwa na wakati mgumu kuwavutia wachezaji endapo haitafuzu kujiunga na Ligi ya Mabingwa.

Mkurugenzi wa AC Milan Frederic Massara amefichua kuwa klabu hiyo bado haijaamua ikiwa itaanzisha mazungumzo ya kumnunua Fikayo Tomori,23, - lakini AC Milan inasisitiza bei ya £26m iliyotolewa na Chelsea iko juu sana.