05 Mar 2021 / 64 views
Ronaldo aweka rekodi nyingine

Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo amecheza mechi ya 600 katika ngazi ya vilabu na kufunga bao la 20 katika Serie A msimu huu walipoishinda Spezia 3-0.

Mabao yote matatu yalifungwa katika kipindi cha pili huku Ronaldo akilifunga goli la tatu alipotumia vyema fursa ya kupewa pasi katika dakika ya mwisho.

Alvaro Morata alikuwa amefunga bao la kwanza kutumia krosi ya mwenzake Federico Bernardeschi kabla ya Federico Chiesa kufunga goli la pili.

Ushindi huo sasa umeisongesha Juventus hadi alama tatu chini ya nambari mbili AC Milan katika Jedwali la Serie A.

Bao la Ronaldo sasa linamaanisha anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga takriban mabao 20 katika kila vipindi 12 vya ligi tano kubwa za bara ulaya.