04 Mar 2021 / 75 views
AC Milan yaisogelea Inter

Klabu ya AC Milan ipo nyuma kwa alama nne dhidi ya Inter Milan anayeongoza msimamo wa ligi kuu soka nchini Italia baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Roma.

Franck Kessie aliipa AC Milan uongozi kwenye mechi hiyo baada ya kushinda goli la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Davide Calabria kufanyiwa makosa kwenye eneo la hatari kwenye mechi hiyo.

Roma kwenye mechi hiyo ilisawazisha goli hilo kupitia Jordan Veretout baada ya kupiga shuti kutoka yadi 18 na kufanya matokeo kuwa 1-1 dakika ya 50.

Baada ya Zlatan Ibrahimovic kutoka nje kutokana na jeraha la kinena, Milan walipata goli la pili dakika ya 58 kupitia Ante Rebic na kufanya matokeo kuwa 2-1 mpaka dakika za mwisho za mchezo huyo.

AC Milan watacheza dhidi ya Manchester United kwenye michuano ya Europa League hatua ya 16 bora ambapo mzunguko wa kwanza utachezwa machi 11 huku mzunguko wa pili ukifanyika machi 18 mwaka huu.