05 Mar 2021 / 78 views
Henderson apata majeraha

Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 10 baada ya kupata majeraha ya kinena kwenye mechi ya ligi dhidi ya Everton.

Kiungo huyo wa England mwenye umri wa miaka 30 alitoka nje kipindi cha kwanza kwenye mechi hiyo waliyofungwa 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa Merseyside.

Baada ya kupata majeruhi hayo mchezaji huyo ameungana na wachezaji wenzake ambao ni majeruhi Virgil van Dijk, Joel Matip, Joe Gomez na Fabinho.

Henderson anatarajiwa kufanyiwa upasuaji na utakaosababisha kukosa mechi za kufuzu kwa kombe la Dunia kwa nchini yake ya England zitakazoanza hivi karibuni.

Kiungo huyo alikuwa anatumika kwenye ulinzi hivi karibuni kutokana na wachezaji wa nafasi hiyo kuwa majeruhi na kusababisha kupoteza mechi kutokana na kuandamwa na majeruhi.

Pia mchezaji huyo atakosa mechi tano za Liverpool pamoja na ya Chelsea katika uwanja wa Anfield pamoja na mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa hatua ya 16 dhidi ya RB Leipzig.