13 Jan 2021 / 25 views
Percy Tau kuanza kuichezea Brighton leo

Percy Tau anatarajiwa kuichezea klabu yake Brighton & Hove Albion watakapocheza na Manchester City kwenye Ligi kuu soka nchini England leo.

Wachezaji wa Brighot Tariq Lamptey, Danny Welbeck, Adam Lallana na Aaron Connolly watakosa mechi hiyo.

Pamoja na majeraha haya yote Graham Potter anaweza kulazimishwa kumpa Percy Tau kuanza pamoja na Neal Maupay baada ya kucheza vizuri siku ya Jumapili.

Manchester City wameshinda mechi zao zote sita za Premier League dhidi ya Brighton & Hove Albion, wakifunga mabao 20 na kufungwa mara mbili tu.

Pep Guardiola amesema kuwa Raheem Sterling yuko fiti kucheza, lakini Aymeric Laporte na Nathan Ake wataendelea kuuguza majeraha yao.

Tangu kuanza kwa 2016/17, Kevin De Bruyne amefunga na kusaidia katika mechi 14 za PL, zaidi ya mchezaji yeyote wa Man City.

Ni Lionel Messi tu ndiye aliyefunga na kusaidia katika mechi nyingi chini ya Pep Guardiola, na 29 Brighton hawajawahi kushinda mechi ya ligi ya ugenini dhidi ya Man City katika mechi 10.

Kocha mkuu wa Brighton Graham Potter ana uwiano wa ushindi wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa asilimia 20 tu toka kuanza kwa ligi hiyo.