13 Jan 2021 / 19 views
Goretzka kukosa mechi ya leo

Kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka ameondolewa kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Ujerumani leo Jumatano dhidi ya Holstein Kiel baada ya kupata majeruha mazoezini.

Bayern, ambao walipoteza mechi yao ya pili ya ligi msimu huu Jumamosi kwa kuchapwa 3-2 na Borussia Moenchengladbach, wana hamu ya kurudia na ushindi na uwezekano wa kuwa karatasi yao safi ya kwanza katika mechi 10.

"Leon Goretzka amepata majeraha na hatosafiri na timu kwenda Kiel," klabu hiyo ilisema leo Jumatano.

Bayen Munich ambao walishinda mataji matano mnamo 2020 bado wako juu ya msimamo wa Bundesliga na hadi 16 ya Ligi ya Mabingwa.

Holstein Kiel kwa sasa wako katika nafasi ya tatu katika ligi ya Bundersliga two hivyo mechi hiyo hatakuwa ngumu sana kutokana na ubora wa vikosi hivyo.