13 Jan 2021 / 31 views
Everton yapanda nafasi ya nne EPL

Everton wamepata ushindi wa sita kutoka kwa mechi tisa za ugenini msimu huu baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Wolvehampton kwenye mechi ya ligi kuu England.

Baada ya ushindi huyo Everton wamepanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini England.

Goli la ufunguzi kwenye mechi hiyo lilifungwa na Alex Iwobi huku goli la kusawazisha la Wolve likifungwa na Ruben Neves kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Wolve walionekana kuwa vizuri katika kipindi cha pili lakini kichwa cha Keane kwenye dakika ya 77 kiliipa ushindi wa alama tatu kikosi cha Carlo Ancelotti.

Everton imeingia kwenye nne bora na alama 32 kutoka kwa michezo 17 wakati Wolves ilishuka hadi nafasi ya 14 ikiwa na alama 22.

Tulikuwa na wachezaji wachache waliokosekana leo lakini tulionyesha nguvu ya kikosi," beki huyo wa zamani wa Burnley Kean alisema.

Nilidhani vijana hawa walifanya vizuri sana, kila mtu alifanya soksi zake mbali." Everton wamefunga mabao tisa ya kichwa msimu huu, zaidi ya timu nyingine yoyote.