13 Jan 2021 / 37 views
Tetesi za usajili Ulaya

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anafiikria kumrudisha meneja wa zamani Avram Grant katika uwanja wa Stamford Bridge ili kumsaidia mkufunzi Frank Lampard.

Real Madrid inapanga kuwauza wachezaji sita msimu huu ili kuchangisha fedha za kumsaini mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe, 22. Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, beki wa kushoto wa Brazil Marcelo, Mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic na wachezaji watatu wa Uhispania Isco, Dani Ceballos na Brahim Diaz ndio wachezaji wanaolengwa.

Beki wa Manchester United Timothy Fosu-Mensah, 23, anatarajiwa kuhamia katika klabu ya Bayer Leverkusen kwa dau la £1.5m baada ya kukataa kuongezewa mkataba katika uwanja wa Old Trafford. 

Wolves haitamnyatia mshambuliaji anayelengwa na kocha Nuno Espiroto Olivier Giroud na yule wa Liverpool Divock Origi, 25, baada ya klabu hiyo kumwambia kocha huyo kwamba haina fedha za kutumia Januari.

Bayern Munich inatarajiwa kumsaini beki wa Reading mwenye umri wa miaka 22 Omar Richards kwa mkataba usio rasmi wakati ambapo inasubiri kandarasi yake kukamilika katika msimu wa joto.. Everton na West Ham zilikuwa na hamu ya kumsajili.

Kiungo wa kati Fernandinho, 35, huenda akaongeza kandarasi yake katika klabu ya Manchester City kwa kuwa hana uhakikia iwapo akubali ofa kutoka Ulaya na Marekani ya latini wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu wa joto.

Beki wa Napoli Kalidou Koulibaly - amehusishwa pakubwa na uhamisho wa Liverpool, Manchester City na Manchester United - atauzwa katika dirisha la uhamisho la mwezi huu iwapo timu itatoa ofa ya £100m kumnunua mchezaji huyo wa senegal mwenye umri wa miaka 29.