13 Jan 2021 / 43 views
Solskjaer awapongeza wachezaji wake

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa vijana wake wana akili na juhudi kubwa ndani ya uwanja jambo ambalo linampa furaha.

Kocha huyo ameongeza kuwa ushindi ambao wameupata mbele ya wapinzani wao unawapa nguvu ya kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo na anaamini watakuwa vizuri.

Manchester United ilishinda bao 1-0 dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Turf Moor na kuwafanya waongoze ndani ya Ligi Kuu England wakiwa na pointi 36 wakiwashusha mabingwa watetezi, Liverpool wenye pointi 33.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Paul Pogba dakika ya 71 ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo.

Ole amesema:"Vijana wamefanya kazi nzuri na kwa juhudi kubwa, hapo walipo wanastahili pongezi kwani sikutarajia kuona uwezo huo, imani yangu ni kwamba wataendelea kuwa bora muda wote ndani ya uwanja,".