21 Nov 2020 / 8 views
Sababu ya Man United kutoshinda Old Trafford

Manchester United imekuwa na rekodi mbaya ya nyumbani kwenye Ligi kuu England msimu huu ambapo kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer amesema kukosekana kwa mashabiki ndani ya Old Traford ndiyo sababu ya timu hiyo kufanya vibaya.

Manchester United bado haijashinda nyumbani msimu huu ikiwa na vipigo vitatu katika michezo minne, pamoja na kupigwa kwa goli 6-1 na Tottenham Hotspur.

Arsenal pia walidai ushindi wao wa kwanza kwa miaka 14 kwenye uwanja huo ambao kawaida hujaa mashabiki 75,000.

United watachuana na West Bromwich Albion ambao hawajapa ushindi toka kuanza kwa ligi ya England msimu huu.

Solskjaer aliwaambia waandishi wa habari. "Michezo dhidi ya Chelsea (0-0) na Arsenal ilikuwa michezo ya karibu sana ambapo nina uhakika wa asilimia 100 ikiwa tungekuwa na mashabiki wetu tungeshinda michezo hiyo.

United ambao wameshinda mechi zote tatu za ugenini hadi sasa, wako nafasi ya 14 kwenye msimamo wakiwa na alama 10 na mchezo mmoja mkononi.