21 Nov 2020 / 57 views
Tetesi za usajili Ulaya

Tottenham huenda ikawasajili wachezaji zaidi mwezi Januari na inatarajiwa kumtafuta mlinzi mpya wa safu ya kati, huku mchezaji wa kimataifa wa Colombia Davinson Sanchez, 24, akitarajiwa kuondoka.

Kiungo wa kati wa Mbrazil Willian, 32, 'amechukuliwa hatua' na Arsenal baada ya kwenda Dubai wiki kadhaa zilizopita - huku Mikel Arteta akisisitiza suala hilo 'limesuluhishwa'.

Jurgen Klopp anasisitiza kuwa hana habari kuwa mabingwa wa Ligi ya Premia Liverpool, wanapania kumnunua mlinzi mpya mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa.

Liverpool wamefahamishwa kuwa watalazimika kulipa £26.7m ikiwa wanamtaka mlinzi wa Ajax Perr Schuurs, 20, huku AC Milan pia wakionesha nia ya kutaka kumnunua mholanzi huyo anayecheza safu ya kati na nyuma.

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti amepuuzilia mbali tetesi zinazoashiria anawataka wachezaji wake wawili wa zamani; kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Isco, 28, na kiungo wa kati wa Juventus na Ujerumani Sami Khedira.

Kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 28, hana mpango wa kuondoka Arsenal kuelekea Inter Milan mwezi Januari.

Kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez amepiga ripoti kwamba alihusika katika ugomvi alipokuwa katika shughuli ya kimataifa katika chumba cha kubadilisha nguo. Mchezaji huyo wa Everton aliripotiwa kugombana na wachezaji wenzake wa kimataifa Jefferson Lerma, 26, wa Bournemouth na Davinson Sanchez, 24 wa Tottenham.

Baba yake Erling Haaland, Alf-Inge, kiungo wa kati wa Nottingham Forest, Leeds na Manchester City, amekiri kuwa mwanawe ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Norway, 20, anatamani kujiunga Ligi ya Premier lakini kwanza anataka kushinda taji na klabu yake ya sasa, Borussia Dortmund.

Kiungio wa kati wa zamani wa Manchester City Trevor Sinclair, anaamini kuwasilia kwa mchezaji nyota wa Barcelona Lionel Messi, 33, 'hakutaepuki' baada ya mkataba wa mkufunzi wa City Pep Guardiola kurefushwa.

Chris Smalling,30, ameilaumu Manchester United kwa kutompatia maelezo dhahiri kuhusu hatma yake kabla ya kumwachilia kwenda Roma mwaka jana, lakini mlinzi huyo wa zamani wa old former England anasema kuwa anafurahia muda Italia.