21 Nov 2020 / 61 views
Takwimu za Benzema ndani ya Madrid

Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema ni mchezaji mwenye mafanikio ndani ya kikosi cha Real Madrid toka alipoondoka mshambuliaji Cristiano Ronaldo iliaminika kuwa timu hiyo itayumba.

Pamoja na kuondoka staa huyo bado Benzema ameonekana kuwa kwenye chati ya juu sana pamoja na kwamba hapewi sifa inayostahili.

Benzema amecheza Real Madrid kwa kipindi kirefu na amefanikiwa kupata makombe kadhaa akiwa na timu hiyo na ni mmoja kati ya washambuliaji waliokaa kwenye timu hiyo kwa muda mrefu.

 

CHINI NI TAKWIMU ZA STAA HUYO KWENYE KIKOSI CHA MADRID;

Umri: Miaka 32

Misimu aliyokaa Real: 11

Mabao aliyofunga Real: 255

Michezo aliyocheza Real: 524

Wastani wa mabao kwa msimu: 20

Makombe aliyotwaa Real: 18

Makombe la Liga: 3

Makombe ligi ya Mabingwa: 4

Jumla ya timu alizochezea: 2

Jumla ya mechi zote: 692

Jumla ya mabao: 336

Michezo timu ya Taifa: 81

Mabao timu ya Taifa: 27