20 Nov 2020 / 69 views
Neymar kurudi kucheza dhidi ya Monaco leo

Mshambuliaji wa PSG, Neymar yuko tayari kurudi kuichezea klabu yake kwenye mechi ya ligi kuu Ufaransa leo dhidi ya Monaco.

Pia Neymar anaweza kurejea kucheza kwenye ligi ya mabingwa dhidi ya RB Leipzig wiki ijayo baada ya kukosekana kwenye mechi iliyopita ya ligi ya mabingwa.

Kocha Thomas Tuchel alisema Alhamisi kwamba Neymar anaweza kucheza "dakika chache" dhidi ya Monaco. Jeraha hilo lilimwondoa kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia la Brazil wakati wa mapumziko ya kimataifa.

PSG, waliomaliza fainali msimu uliopita, wanahitaji kuifunga Leipzig nyumbani Jumanne ili kubaki kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu kwa hatua ya mtoano.

Kylian Mbappe pia amerejea katika kikosi cha PSG licha ya kusumbuliwa na majeraha tangu mwanzo wa msimu.

Marco Verratti na Mauro Icardi bado hawako tayari kurudi kutoka majeruhi lakini Kocha wa PSG, Thomas Tuchel alisema alikuwa na matumaini watapatikana kwenye mechi dhidi ya Leipzig.