20 Nov 2020 / 271 views
EPL kurejea mwisho wa wiki hii

Ligi kuu ya England inarejea tena kesho kwa michezo minne baada ya kusimama kwa muda wa wiki mbili kupisha michezo mbalimbali ya timu za taifa ambazo zimemalizika.

Chelsea watakuwa ugenini kuchuana na Newcastle United kwenye dimba la St.James lenye historia mbovu na Chelsea tokea mwaka 2004 ambapo The Blues wameshinda mchezo mmoja pekee, sare 2 na vipigo 3 kwenye michezo 5 ya mwisho ya EPL.

Chelsea wanatazamiwa kuwakosa wachezaji wake nyota Christian Pulisic na Kai Havertz ambao wanasumbuliwa na majeraha wakati Callum Wilson wa Newcastle akiwa fiti.

Newcastle Utd, Mshambuliaji wake wakutumainiwa Callum Wilson mwenye mabao 6 na kutengeza 1 kwenye michezo 7 anatarajiwa kuwepo dimbani.

Mara ya mwisho wawili hawa kukutana ilikuwa ni tarehe 18 mwezi januari mwaka huu ambapo Newcastle walipata ushindi wa bao 1-0 kwenye dimba lake la nyumbani kwenye mchezo wa EPL.

Aston Villa watachuana na Brighton waliopo nafasi ya 16 mishale ya saa 12 kamili jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki kwenye dimba la Villa park.

Mchezo unaosubiriwa na wapenzi wengi wa soka hapo kesho ni ule utakaowakutanisha Tottenham Hotspurs na Manchester City utakaochezwa katika uwanja wa Tottenham Hotspurs.

Manchester United dhidi ya West bromwich Albion ni mchezo mwingine wa EPL utakaopigwa hapo kesho wenyewe ukitazamiwa kuchezwa saa 5 mashetani wekundu imepoteza 3 na sare 1 na kushinda michezo 3 ugenini.