20 Nov 2020 / 68 views
Romeu asaini mkataba mpya

Kiungo wa Southampton, Oriol Romeu amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na nusu ambayo itamuweka klabuni hapo hadi majira ya joto ya 2023.

Mhispania huyo wa miaka 29 alikuwa ameingia msimu wa mwisho wa makubaliano yake ya sasa kwenye klabu hiyo na kuamua kusaini mkataba mpya.

Kiungo huyo wa zamani wa Barcelona Romeu amecheza mara 198 kwa Watakatifu tangu ajiunge kutoka klabu ya Chelsea mnamo 2015.

"Sijaona wachezaji wengi ambao ni wataalamu kama Oriol wakati wangu kama meneja," alisema meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl.

"Anajitolea kabisa katika kila kitu anachofanya, iwe ni kwenye mazoezi au kwenye mechi, na huu ni mfano mzuri wa kwa wachezaji wengine."