20 Nov 2020 / 62 views
Virgil Van Dijk aanza mazoezi

Beki wa Liverpool, Virgil Van Dijk anatajwa kuanza kufanya mazoezi mepesi yatakayomsaidia kurejea kwenye ubora wake wa zamani.

Beki huyo wa kati anasumbuliwa na majeraha ya goti ambapo kwa sasa anapambana ili arejee uwanjani baada ya kuumizwa na nyota wa Everton, Jordan Pickford kwenye Merseyside dabi mwezi uliopita

Baada ya kufanyiwa vipimo na upasuaji Van Dijk taarifa zinaeleza kuwa ameanza kufanya mazoezi mepesi ambayo yatamfanya aweze kurejea kwenye kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England chini ya Jurgen Klopp.

Taarifa kutoka Liverpool imeeleza kuwa beki huyo anaendelea vizuri na upasuaji wake ulikwenda vizuri jambo ambalo limemfurahisha Klopp ambaye amesema kuwa wanatarajia kuwa na habari njema hivi karibuni.

Liverpool inapambana kutetea taji la ligi ikiwa inawakosa nyota wake wengi ambao ni mabeki ikiwa ni pamoja na Joe Gomez, Fabinho ambao wanasumbuliwa na majeraha.