17 Oct 2020 / 66 views
Debrune kuwakosa Arsenal

Kocha wa timu ya Manchester City, Pep Guardiola, amethibitisha kuwa mkali wa ‘assist’ Kevin de Bruyne ‘KDB’ hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza na Arsenal leo usiku, saa 1:30,  kutokana na kupata majeraha kwenye timu ya taifa ya Ubelgiji.

“Majeraha yake si makubwa sana, unajua Kevin amecheza mechi nyingi bila kumpunzika kwenye timu ya taifa na klabu, pia hakuwa na ‘pre season’ kwa hiyo mwili nao huwa unachoka kutumika sana mpaka amepata majeraha lakini si makubwa, atarudi hivi karibuni,” alisma kocha huyo.

KDB pia ataikosa mechi ya ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto ya Ureno siku ya Jumatano lakini habari njema ni kuwa mshambuliaji namba moj,a Sergio Aguero, yupo fiti baada ya kupona majeraha na anatarajiwa kuiongezea makali safu ya ushambuliaji ya Manchester City.

Arsenal wamezidi kuimarisha kikosi chao hasa baada ya usajili wa kiungo mkabaji, Thomas Partey, waliyemsajili kutoka Atletico Madrid ya Hispania.

Huu ni usajili bora zaidi kufanywa kwenye eneo la kiungo mkabaji  tangu kuondoka kwa aliyekuwa nahodha wao Mfaransa  Patrick Viera.   The Gunners wameonekana kushindwa kupata mbadala wake kwa miaka mingi.