19 Oct 2020 / 74 views
Zabaleta astaafu soka

Beki wa kulia wa Argentina Pablo Zabaleta ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 35 baada ya kucheza mpira kwa kipindi cha miaka 18 hadi alipoamua kustaafu.

Zabaleta amechezea San Lorenzo, Espanyol, Manchester City na West Ham United katika kipindi cha miaka 18 ya uchezaji soka na sasa ameamua kutundika daruga katika mchezo wa soka.

Zabaleta alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu pamoja na Kombe la FA na Mataji mawili ya Ligi akiwa na Manchester City kutoka 2008 hadi 2017 na kuhamia West Ham United.

Alicheza pia michezo 58 kwa nchi yake wakati alikuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kwenye Kombe la Dunia la 2014, akisaidia taifa lake kufika fainali na kufungwa na Ujerumani. ..