16 Oct 2020 / 73 views
Neymar kukosa mechi ya PSG leo

Mshambuliaji wa PSG, Neymar atocheza mechi ya Ligi dhidi ya Nimes leo kutokana uchovu wa safari kutoka Brazil hadi nchini Ufaransa.

Mchezaji huyo ghali zaidi duniani alifunga hat-trick kwa nchi yake katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Peru kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Mechi hiyo katika mji wa Lima ilimalizika muda mbaya kwa saa za Ulaya na mabadiliko ya haraka inamaanisha hatacheza mechi wikendi hii.

Kocha wa Paris Thomas Tuchel amesema kuwa mchezaji huyo atacheza mechi ya Jumanne ya ligi ya mabingwa dhidi ya Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani.

PSG haitakuwa na wachezaji wake muhimu kwenye mechi dhidi ya Nimes ambapo wanatafuta ushindi wa tano mfululizo baada ya kuanza msimu kwa kufngwa mechi mbili mfululizo.

Angel Di Maria na Marquinhos wamesimamishwa kutokana na adhabu wakati Marco Verratti na Mauro Icardi ni miongoni mwa wachezaji walikuwa na majeraha.

Kiungo Danilo Pereira lazima asubiri mchezo wake wa kwanza baada ya kufika kwa mkopo kutoka Porto na amejitenga baada ya kuwasiliana na Cristiano Ronaldo, ambaye amekutwa na Covid-19.

Wachezaji wapya Rafinha na Moise Kean wanaweza kucheza, na Kylian Mbappe yuko kikosini licha ya kuichezea Ufaransa huko Croatia Jumatano jioni.