16 Oct 2020 / 69 views
Wenger alivyomkatalia Van Persie

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amefichua kuwa alimkatalia mshambuliaji Robin Van Persie kurejea katika klabu ya Arsenal kutokea Manchester United mwaka 2015.

Van Persie alikuwa na miezi sita ya kwanza mizuri Old Trafford, aliwaweka katika mstari wa Ubingwa wa ligi kuu na kufanya kuwa vigumu zaidi kwetu sisi” ameandika Wenger katika kitabu chake kipya kiitwacho My Life In Red and White”.

Lakini baada ya miaka mitatu katika minne aliyoisaini, alipata majeraha na (Van Gaal) alimuuza kwenda Uturuki Fenerbahçe.”

Alinipigia kwa sababu alitaka kurudi, lakini haikuwezekana . Alikuwa mwishoni mwa soka lake na tulikuwa tunawekeza katika wachezaji wadogo.