16 Oct 2020 / 69 views
Ibrahimovic kurejea uwanjani

Mshambuliaji wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic anajiandaa kurudi kwenye mechi ya Jumamosi ya Milan dhidi ya Inter Milan kwenye ligi kuu soka nchini Italia Seria A.

Ibrhahimovic amepona na anategemea kurudi uwanjani baada ya mechi dhidi ya Bologna kabla ya kukutwa na ugonjwa wa Corona.

Msweden huyo hajacheza mchezo tangu tarehe 21 Septemba, lakini aliendelea kufanya mazoezi makali wakati wa kutengwa.

Licha ya kukosekana kwake, Milan wameanza msimu mzuri, wakiwa wamepanda hadi nafasi ya pili, na kushinda mechi tatu kutoka kwa michezo mitatu na kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Europa.

Kikosi cha Stefano Pioli kipo nafasi ya pili nyuma ya Atalanta, ambao pia wamepata ushindi mara tatu, lakini mabao 13 ya kuvutia yamefungwa.

Inter Milan, wakati huo huo, ina wachezaji sita wakiwa wamejitenga baada ya kukutwa na virusi vya Corona ambao ni Ashley Young, Alessandro Bastoni, Milan Skriniar, Radja Nainggolan, Roberto Gagliardini na Ionut Radu.

Kikosi cha Antonio Conte kina alama saba kutoka kwa mechi tatu, Romelu Lukaku na Lautaro Martínez wakifunga mabao sita kati ya 10 ya Inter hadi sasa.